Maajabu saba(7) ya dunia (Asilia)
Dunia inamaajabu mengi na imejaa maajabu mazuri na yakushngaza yanayovutia watu kote ulimwenguni.Maajabu yake yanagawanyika katika makundi mawili, Maajabu ya asili ambayo yametokana kutokana na nguvu za asili na Maajabu ya kibinadamu ambayo yamejengwa na wanaadamu kwa maarifa na ustawi wa hali ya juu. Ili kuyajua hayo tuangalie maajabu hayo saba Kati ya Maajabu ya asili na Maajabu ya kibinadamu, Maajabu ya asili 1.Mlima everest (Nepal/Tibel) - Mlima Everest unajulikana kama Chomolungma (kwa Tibet) na Sagarmatha (kwa Kinepal), ni mlima mrefu zaidi duniani juu ya usawa wa bahari. Uko katika safu ya milima ya Himalaya kwenye mpaka kati ya Uchina na Nepal. Sifa mojawapo wa MLIMA huu unaurefu wa miita 8,848.86 (futi 29,031.7).Mlima Everest ni maarufu kwa kuwa changamoto kubwa kwa wapandaji milima. Kupanda kilele chake kunahitaji maandalizi makubwa, uzoefu, na vifaa maalum ili kufanikisha kufika kileleni. Mlima everest 2.Grand canyon ( ma...