MAAJABU YA KABILA LA WAHADZABE

Tanzania🇹🇿 ni nchi mojawapo barani Africa yenye utajiri mkubwa sana wa utamaduni,Ikiwa na takribani makabila 120 ndani yake na miongoni mwa makabila haya mojawapo ni Wahadzabe wanaopatikana maeneo ya ziwa Eyasi karibu na hifadhi ya taifa ya Serengeti.Wahadzabe ni kabila dogo sana lakini lenye urithi wa kipekee wa maisha ya  uwindaji, na ukusanyaji matunda,Wakihifadhi mtindo wa maisha ya zamani kwa maelfu ya miaka iliopita.
Wataalamu wanasema jamii hii ilikuwepo kwa zaidi ya miaka 10,000 ikiendelea kuhifadhi mtindo wao wa maisha bila kutegemea kilimo wala ufugaji.
Mwanaume wa kabila la wadzabe akichonga mshale 





Lugha wanayotumia jamii ya Wahadzabe ni lugha ijulikanayo kama Hadza,ambayo ni yakipekee kwakuwa inasauti za "klik" kama zile zinazopatikana kwenye lugha za Khoisan za kule Afrika kusini. Sifa nyingine ya lugha hii ni kwamba haina uhusiano wowote na lugha yoyote Kati ya zilizopo hapa Tanzania.


Maisha ya Kila siku ya Wahadzabe 

Wahadzabe wanaishi kwa kuwinda wanyama na kukusanya matunda, mizizi, na asali. Hawana mashamba, hawafugi mifugo, wala hawajihusishi sana na biashara. Wanaume ndio wawindaji wakuu, hutumia mishale na upinde kuwinda wanyama kama swala, nyani, na ndege. Wanajulikana kwa uwezo wao wa hali ya juu wa kufuatilia nyayo za wanyama na kujua tabia za wanyama kwa kina.

Kwa upande mwingine, wanawake huhusika zaidi na ukusanyaji wa matunda, mizizi, na mbegu. Asali ni moja ya vyakula wanavyothamini sana, na mara nyingi huifuata kwa kushirikiana na ndege waitwao "Honeyguides" wanaowaonyesha mahali panapopatikana asali porini
Mizizi itumiakayo kama chakula na kabila la wadzabe 

Asali moja ya chakula pendwa kwa kabila la wadzabe 

Wahadzabe hawana makazi maalumu ya kuishi.Wanaishi kwenye mapango au kwenye nyumba za muda zilizotengenezwa kwa majani hivyo wakinaliza rasilimali za eneo husika wanahama na kuhamia sehemu nyingine ambazo watapapa chakula na mahitaji yao ya siku zote

Nyumba za wahadzabe zilizotengenezwa kwa nyasi na magome makavu

Jamii hii haina viongozi rasmi, na maamuzi hufanywa kwa makubaliano ya pamoja. Hawana utawala wa kifalme wala serikali ya kikabila, jambo linalowafanya kuwa jamii yenye usawa mkubwa kuliko makabila mengine mengi.
Safari ya kutembelea Wahadzabe ni fursa adimu ya kuona jamii inayoishi kama binadamu wa zamani walivyokuwa wakiishi. Wageni wanaweza kujifunza jinsi ya kuwinda kwa upinde na mshale, kuonja asali yao ya asili, na kushuhudia mfumo wao wa maisha wa kushirikiana bila mgawanyiko wa madaraja ya kijamii.
Ikiwa unapenda utalii wa kipekee na wa kitamaduni, basi kutembelea Wahadzabe ni mojawapo ya safari bora kabisa nchini Tanzania. Unapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa jamii inayothamini urithi wake wa zamani na inayoendelea kuishi kwa njia ya asili licha ya mabadiliko ya dunia.

Pia unaweza kujisomea kwa undani zaidi kuhusu kabila la hadzabe linalopatikana nchini Tanzania kwa kununua kitabu Amazon,Ikiwa unahitaji kitabu hiki bofya Hapa

Ingawa utalii umewaleta kipato, wakati mwingine unahatarisha utamaduni wao, kwani baadhi ya wageni hujaribu kubadilisha mtindo wao wa maisha.

Ukitaka kujua kuhusu kabila la Maasai bofya Hapa


Comments

Popular posts from this blog

WANYAMA 10 WANAOTISHA ZAIDI PORINI ( Usiombe kukutana nao❌)

🧳 Top 10 Travel Games to Keep Kids Entertained on the Go

The Benefits of Visiting Tourist Attractions Around the World