Maajabu saba(7) ya dunia (Asilia)
Dunia inamaajabu mengi na imejaa maajabu mazuri na yakushngaza yanayovutia watu kote ulimwenguni.Maajabu yake yanagawanyika katika makundi mawili,Maajabu ya asili ambayo yametokana kutokana na nguvu za asili na Maajabu ya kibinadamu ambayo yamejengwa na wanaadamu kwa maarifa na ustawi wa hali ya juu.
Ili kuyajua hayo tuangalie maajabu hayo saba Kati ya Maajabu ya asili na Maajabu ya kibinadamu,
Maajabu ya asili
1.Mlima everest (Nepal/Tibel) - Mlima Everest unajulikana kama Chomolungma (kwa Tibet) na Sagarmatha (kwa Kinepal), ni mlima mrefu zaidi duniani juu ya usawa wa bahari. Uko katika safu ya milima ya Himalaya kwenye mpaka kati ya Uchina na Nepal.
Sifa mojawapo wa MLIMA huu unaurefu wa miita 8,848.86 (futi 29,031.7).Mlima Everest ni maarufu kwa kuwa changamoto kubwa kwa wapandaji milima. Kupanda kilele chake kunahitaji maandalizi makubwa, uzoefu, na vifaa maalum ili kufanikisha kufika kileleni.
![]() |
| Mlima everest |
2.Grand canyon (marekani)
Grand Canyon ni korongo kubwa lililochongwa na Mto Colorado huko Arizona marekani. Ni mojawapo ya maajabu ya asili ya dunia, inayojulikana kwa ukubwa wake mkubwa, kina, na miamba ya rangi.
Grand Canyon ni hifadhi ya Taifa na imekuwa kivutio maarufu cha watalii kwa zaidi ya karne moja. Hifadhi hiyo inatoa shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupanda mlima, kuendesha baiskeli, kuendesha farasi, na kuendesha mashua.
Ikiwa unapanga kutembelea Grand Canyon, kuna mambo machache unayopaswa kujua:
* Hifadhi hiyo iko wazi mwaka mzima, lakini hali ya hewa inaweza kutofautiana sana. Joto la majira ya joto linaweza kufikia zaidi ya 100°F (38°C), wakati joto la majira ya baridi linaweza kushuka chini ya 0°F (-18°C).
* Kuna rims mbili za Grand Canyon: South Rim na North Rim. South Rim iko wazi mwaka mzima, wakati North Rim imefungwa wakati wa majira ya baridi.
* Kuna njia nyingi za kupanda mlima na maeneo ya kambi ndani ya hifadhi. Ikiwa unapanga kupanda mlima au kambi, unapaswa kupata kibali kutoka kwa Hifadhi ya Taifa.
![]() |
| Grand canyon |
3.Amazon rainforest (Amerika kusini)
Msitu wa Amazon ni msitu mkubwa wa mvua duniani. Unapatikana katika bara la Amerika Kusini, na unajumuisha sehemu za nchi tisa: Brazil, Peru, Colombia, Venezuela, Ecuador, Bolivia, Guyana, Suriname na French Guiana. Msitu huu una eneo la kilomita za mraba milioni 7, na ni nyumbani kwa viumbe vingi vya aina yake.
Msitu wa Amazon una jukumu muhimu katika kudhibiti hali ya hewa duniani, na pia ni chanzo muhimu cha oksijeni. Hata hivyo, msitu huu unakabiliwa na tishio kubwa la ukataji miti, ambao unasababishwa na shughuli za kilimo, ufugaji na uchimbaji wa madini. Ukataji miti una athari kubwa kwa viumbe na mazingira, na pia unachangia mabadiliko ya tabianchi.
Juhudi mbalimbali zinafanywa kulinda msitu wa Amazon, ikiwa ni pamoja na kuweka sheria na kanuni za kulinda misitu, kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa msitu, na kusaidia maendeleo endelevu ya jamii zinazoishi karibu na msitu.
![]() |
| Amazon forest |
Victoria Falls ni maporomoko ya maji kwenye Mto Zambezi, kwenye mpaka kati ya Zambia na Zimbabwe. Ni moja ya maporomoko makubwa zaidi duniani, ikiwa na upana wa mita 1,708.
Victoria falls pia inajulikana kwa jina la asili la kiafrika "Mosi-oa-tunya" lenye maana ya moshi unaounguruma.
![]() |
| Victoria falls |
5.Paricutin (mexico)
Paricutin ni volcano ambayo ilitokea mnamo mwaka 1943 huko mexico kwenye shamba la mkulima.Mlipuko wa paricutin ulikuwa ni tukio kubwa la kiolojia ambalo lilivutia umati mkubwa wa wanasayansi.Uliwawezesha wanasayansi kuchungiza mzima wa volcano kiujumla tangu kuanza kwake hadi kuzima kwake.
Mlipuko wa paricutin ulizika au kufunika vijiji viwili na kufanya mamia ya watu kupoteza makazi yao.Hata ivyo ilifanya mazingira kuonekana tofauti hata kupelekea watu kutoka sehemu tofauti duniani kufika eneo hilo kujionea maajabu hayo
![]() |
| Paricutin (Mexico) |
6.Aurora borealis (kaskazini mwa Dunia)
Ni mwanga wa ajabu unaong’aa angani wakati wa usiku, hususan katika maeneo ya Aktiki.Unasababishwa na chembe kutoka kwenye jua kugongana na anga ya dunia.
Rangi zake za kijani, bluu, na zambarau huonekana vizuri zaidi katika nchi kama Norway, Kanada, na Iceland.
![]() |
| Aurora borealis |
7.Bahari iliyokufa ( Dead sea-Israel/Jordan/Palestina)
Dead sea ni bahari yenye chumvi nyingi kiasi kwamba hakuna kumbe yoyote anaeweza kuishi huko.
Bahari iliokufa inahistoria tajiri na imetajwa hata kwenye biblia,Pia watu wamekuwa wakienda kwenye bahari iliyokufa ili kujifaidisha na madini yake mengi ambayo inaaminika kuwa ni mali na uponyaji
![]() |
| Picha ikinmuonyesha mtu akielea kwenye bahari yenye chumvi |
Bahari iliokufa ni hazina ya kipekee ya asili ambayo inaoaswa kulindwa kwa vizazi na vizazi.Ni muhimu kwamba hatua madhubuti zichukuliwe sasa ili kuhakikisha kwamba Bahari iliokufa inaendelea kuwepo na kustawi.
Tutaendelea na Maajabu ya kibinadamu......














Comments