Mji wa Jerusalem na milki zake
Jerusalem na kubadili jina kutoka Yudea (Judea) kuwa Palaestina. Hili ni jina la Kigiriki lililolenga kuondoa muungano wowote walionao Wayahdi kwenye eneo hilo. Wayahudi wote walipigwa marufuku kukanyaga Jerusalem.
Baada ya kuondolewa Yudea, Wayahudi walisambaa katika maeneo mbalimbali yaliyokuwa chini ya utawala wa Kirumi, Ulaya ya leo. Lakini walishambuliwa kila sehemu walipoenda.
Katika karne ya 11, Wayahudi waliuawa na wapigania Kristo (Crusaders) kwa kigezo kwamba wao ndio walimuua Yesu. Kwenye karne ya 14, Wayahudi waliuawa kwa madai kwamba wao ndio chanzo cha vifo vinavyojulikana kama black death. Walituhumiwa kwa kubadili mahubiri ya Yesu na kushambilia majeshi ya Warumi.
Wayahudi waliendelea kushambuliwa mpaka karne ya 19 ambapo baadhi ya Wahudi waliunganisha nguvu ili kulinda chimbuko lao. Walianzisha kitu kinachojulikana kama Zionism. Hii ilikuwa itikadi ya kisiasa, na kidini ambayo ililenga mambo mawili.
1.Ililenga kuzuia Wayahudi kushambuliwa
2.Ililenga kuwarudisha Wayahudi Jerusalem
Wazionist waliamini kwamba Uyahudi sio tu kwamba ni dhehebu, bali ni utaifa. Walidai kwamba Wayahudi hawanabudi kuwa na taifa kama ilivyo kwa Wafaransa walivyo na taifa la Ufaransa. Harakati hizi ndizo ziliwarudisha Israel. Leo hii itikadi ya Zionism ni itikadi ya taifa la Israel.
Kufikia mwisho wa karne ya 19, harakati hizi zilisababisha Wayahudi wengi kwa makundi kuhamia Palestina. Kufikia mwaka 1903, kiasi cha Wayahudi 30,000 walikuwa tayari wameweka makazi yao Palestina. Kufikia mwaka 1914, kulikuwa kuna ongezeko la Wayahudi wengine 40,000.
Hapa sasa ndipo Vita ya kwanza ya dunia ikaanza. Dola ya Ottoman ikaanguka, huku Waingereza na Wafaransa wakiyatawala makoloni ya Asia. Palestina ikawa chini ya Waingereza.
Mwanzoni, Waingereza waliruhusu Wayahudi kuendelea kuhamia Palestina. Lakini, kadri Wayahudi walivyoongezeka mvutano baina ya Waarabu na Wayahudi nao ukaongezeka. Pande zote zilishambuliana huku kila upande ukidai unaonewa. Hivyo, kufikia mwaka 1930, Waingereza walianza kudhibiti Wayahudi kuhamia Palestina.
Kuibuka kwa Nazi – Ujerumani
Mambo yalibadilika tena baada ya kuibuka kwa itikadi ya Nazi. Inakadiliwa kwamba Wayahudi milioni 6 waliuawa. Waliosalia walikimbilia Marekani na Palestina kwa idadi kubwa. Kufikia mwaka 1944, idadi ya Wayahudi wanaoishi Palestina ilifika 33% ya wakazi wote. Hii ilisababisha nchi za magharibi kuanza kuunga mkono kuundwa kwa taifa la Wayahudi. Lakini nchi nyingi za Kiarabu hazikutaka jambo hili litokee.
Mwaka 1947, uadui baina ya Wayahudi na Waarabu uliongezeka. Umoja wa Mataifa ulipitisha mpango wa kuigawa Palestina katika nchi mbili. Moja iwe ya Wayahdi na iitwe Israel na nyingine ibaki kwa ajili ya Waarabu, Palestina. Ambapo Israel iwe na ukubwa wa 56.5% la eneo lote huku Palestina ikibaki na 43.5% ya eneo.
Katiak azimio hilo, mji wa Jerusalem ulipaswa kubaki kuwa eneo la kimataifa kwa kuwa madhehebu yote yanalichukulia kama eneo takatifu. Mpango huu ulishindwa kabisa kufanikiwa.
Waingereza walishindwa kuzuia machafuko, hivyo kujiondoa kabisa na kuwaachia wahusika wadundane wenyewe. Wao waliondoka wakiacha machafuko nyuma. Wayahudi wao walikubaliana na mpango wa Umoja wa Mataifa.
Tarehe 14 Mei, 1948 Wayahudi walidai uhuru wa taifa lao na kuunda taifa lao la Israel. Wapalestina waliona jamb hili ni wizi, na Wayahudi wamewaibia eneo lao. Basi kilichofuata ni migogoro na uadui baina ya Wayahudi na waarabu.
Kwa Zaidi ya miaka 70, wamepigana zidi ya vita 8 zilizo rasmi huku mashambulizi madogo madogo ambayo hayana idadi.
Katika vita hizi na migogoro hizi, Israel aliendelea kujinyakulia maeneo ya Palestina.
![]() |
Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 1947 |
![]() |
| Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 1948, baada ya vita ya Israel dhidi ya Waarabu |
Jerusalem ni moja ya miji maarufu zaidi duniani kwa utalii wa kidini, kihistoria na kitamaduni. Iko nchini Israel na ina umuhimu mkubwa kwa dini tatu kuu: Ukristo, Uislamu, na Uyahudi.
Vivutio vya Kitalii Jerusalem
1. Mji wa Kale wa Jerusalem (Old City)
Ukuta wa Kilio (Western Wall) – Eneo takatifu kwa Wayahudi.
Msikiti wa Al-Aqsa & Dome of the Rock – Moja ya maeneo matakatifu zaidi kwa Waislamu.
Kanisa la Kaburi Takatifu (Church of the Holy Sepulchre) – Mahali ambapo Wakristo wanaamini Yesu alisulubiwa na kufufuka.
Via Delorosa – Njia inayoaminika kuwa Yesu alipitia kuelekea kusulubiwa.
2. Mlima wa Mizeituni (Mount of Olives)
Una mwonekano mzuri wa jiji na maeneo matakatifu.
Pia ni nyumbani kwa Makaburi ya Wayahudi ya miaka 3,000.
3. Mahali pa Kidini na Historia
David’s Tower (Migdal David) – Jumba la kihistoria lenye maonyesho kuhusu historia ya jiji.
Bethlehem (karibu na Jerusalem) – Mahali anapoaminika kuzaliwa Yesu Kristo.
Yad Vashem – Makumbusho ya Holocaust.
4. Soko la Mahane Yehuda (Mahane Yehuda Market)
Mahali pazuri kwa chakula cha Kiyahudi na ununuzi wa bidhaa za kienyeji.
src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhH0wRwa_AIZkPkTV5_tuBDjg4Kw8maUIDeREri5ZGL1svfu2_VRvs1InjcgXSM7jlCKlZCAlRwX7uetwWQrMYl3Ys7ApY-GFG8zXIXG9sOTDxG-Q_4wh_nShmdmRA8xdxDH_cZMj71QnlOWz3nkGL7RlO5SGAVL3Uh5ez8wRe1-1LFmgemr2I466M5Psk/s16000/roxanne-desgagnes-di1tfXuDdOg-unsplash.jpg" />5. Jiji la Kisasa la Jerusalem
Makazi, migahawa, hoteli za kifahari, na maisha ya usiku yanayochangamka.
Mambo ya Kufanya Jerusalem
I.Kutembelea maeneo ya kidini na kihistoria
II.Kujaribu vyakula vya Kiyahudi na Kiarabu
III.Kushuhudia mchanganyiko wa tamaduni na dini
IV.Kufanya ununuzi katika masoko ya kienyeji
Jerusalem ni mji wenye historia ndefu na vivutio vya kipekee kwa watalii wa aina zote, iwe ni wa kidini, kihistoria, au wapenda utamaduni.
π’ Advertise with Us! Looking to promote your brand to travel enthusiasts? We offer banner ads, sponsored posts, and affiliate partnerships. Contact us at alvincalvin021@gmail.com to get started!
Phone number: +255 616152067

.jpeg)







Comments