Siri za maisha ya viumbe wa porini na majini
Katika dunia hii, wanyama wana tabia tofauti zinazowasaidia kuishi katika mazingira yao. Kutoka kwa simba mwenye nguvu hadi chura mdogo, kila mnyama ana sifa za kipekee zinazomwezesha kuishi, kujilinda, au kuwinda chakula.Pia kama haukuweza kusoma makala kuhusu Wanyama 10 Wanaotisha zaidi porini bofya Hapa. Katika makala hii, tutachunguza tabia mbalimbali za wanyama na jinsi zinavyowasaidia kuendelea kuishi maisha yao ya Kila siku
1. Wanyama Wanaolinda Maeneo Yao (Territorial Animals)
Baadhi ya wanyama ni wenye wivu na himaya zao, na hawapendi wageni kwenye maeneo yao. Wanyama hawa hulinda maeneo yao kwa kutumia harufu, sauti, au vita
I.Simba – Ni mnyama anaepatikana katika maeneo mengi sana duniani na akiwa ni kumbe maarufu kufahamika na Kila mmoja,Simba anakadiriwa kuwa na uzito wa 120kg - 250kg (Dume) na 100 - 180 (Jike),Urefu wa 1.4m - 2.5m ila mkia.
![]() |
| Simba dume |
![]() |
| Simba jike |
II.Mbwa-mwitu wa Afrika – Ni mnyama anaepatikana oporini na akiwa na sifa nyingi sana akiwa pia anajulikana kwa jina la Mbwa madoa madoa.
Mbwa mwitu anasifa ya kuwa na masikio marefu yaliyosimama,Huwinda na wenzake kwa pamoja Huweka mipaka ya eneo lao kwa kutumia harufu ya mkojo.
![]() |
| Mbwa mwitu |
III.Nyati – Huwa na tabia ya kushambulia wanyama au binadamu wanaokaribia kundi lao.Nyati pia hujulikana kama Mbogo ni mnyama mkubwa wa Africa na mwenye hatari kubwaa
Nyati anamwili mkubwa na imara,Pembe zilizochongoka pia anarqngi ya kijivu na nyeusi.
Ni mnyama anaekula nyasi na anaependa kuishi kwa makundi makubwa
![]() |
| Nyati |
2. Wanyama Wanaotumia Kujificha (Camouflage Animals)
Wanyama wengine hutegemea kujificha (camouflage) ili kujikinga dhidi ya wanyama wanaowinda au kuwasaidia kuwinda kwa mafanikio.
Mifano:
I.Kinyonga – Kinyonga ni mnyama wa aina ya mjusi. Wao huainishwa katika familia ya Chamaeleonidae ambayo ni sehemu ya oda ya Squamata (mijusi na nyoka) katika ngeli ya Reptilia.Hubadilisha rangi yake kulingana na mazingira.
![]() |
| Kinyonga |
II.Paka-mwitu (Leopard) – Ana madoadoa yanayomfanya asionekane kwa urahisi kwenye nyasi.Anamwili mwembamba na misuli imara,Ana urefu wa wastani wa mita 1 hadi 1.9 (bila mkia) na urefu wa mabega wa sentimita 60-70.
III.Samaki wa Leafy Sea Dragon – Samaki aina ya leafy sea dragon (jina la kisayansi: (Phycodurus eques) ni samaki wa baharini wa ajabu sana na wa kipekee. Hii hapa ni baadhi ya mambo muhimu kuhusu samaki huyu ni muonekano wake,wanafanana sana na majani au mwani unaoelea baharini. Wana viambatisho vingi vinavyofanana na majani yaliyochanua mwili mzima, vinavyowasaidia kujificha vizuri sana katika mazingira yao.
3. Wanyama Wanaotumia Sauti kwa Mawasiliano
Baadhi ya wanyama hutegemea sauti maalum kuwasiliana, kama vile kupatikana kwa chakula, hatari, au wito wa upendo.
Mifano:
I.Tembo – Hutoa sauti ya chini (infrasound) inayoweza kusikika kwa umbali wa kilomita nyingi.
Anakadiriwa kuwa na uzito wa Kati ya tani 4 hadi 7 na urefu Kati ya mita 3 hadi 4.Tembo hula Hadi kilo 150 za chakula ikiwemo majana,matunda na magome ya miti
![]() |
| Tembo (Ndovu) |
II.Nyuki – Nyuki ni wadudu wa jamii ya Hymenoptera wanaojulikana kwa kutengeneza asali na kusaidia katika uchavushaji wa mimea.Nyuki wanazi sifa kadhaa mfano Hutoa milio maalum kuonya wenzao kuhusu hatari,Nyuki hukusanya nekta kutoka kwa maua na kuibadilisha kuwa asali kwa matumizi yao na binadamu.
III.Popo – Hutumia echolocation (sauti ya mwangwi) ili kujua wapi kuna vizuizi au mawindo.
4. Wanyama Wanaoshirikiana (Social Animals)
Wanyama wengine huishi katika jamii na hufanya kazi kwa ushirikiano ili kuishi.
Mifano
I.Nyuki – Hufanya kazi kama jamii na kuwa na malkia, wafanyakazi, na askari.

Nyuki
III.Dolphin – Dolphin (pomboo) ni mnyama wa baharini wa jamii ya cetaceans anayejulikana kwa akili yake ya hali ya juu na tabia yake ya kucheza na ni miongoni mwa Wanyama wanaopenda sana kucheza na binadamu.Hushirikiana na wenzake kusaidiana kutafuta chakula na kujikinga.
Dolphin (Pomboo)
5. Wanyama Wanaolala Muda Mrefu (Hibernating Animals)
Baadhi ya wanyama huingia katika usingizi wa muda mrefu (hibernation) ili kujilinda dhidi ya hali mbaya ya hewa, hasa wakati wa baridi kali.
Mifano:
I.Dubu – Dubu (Bear) ni mnyama mkubwa wa jamii ya Ursidae anayepatikana katika mabara mbalimbali, hasa Amerika Kaskazini, Ulaya, na Asia.Dubu ana mwili wenye misuli mingi, manyoya mazito, na miguu yenye nguvu.
Hukaa miezi kadhaa bila kula, huku mwili wake ukitumia mafuta yaliyohifadhiwa.
![]() |
| Dubu (bear) |
![]() |
| Chura wa alaska |
Tabia za wanyama ni za kushangaza na za kuvutia. Kila aina ya mnyama ana njia zake za kuishi, kupambana na hatari, na kupata chakula. Ulimwengu wa wanyama ni wa ajabu, na tunapojifunza zaidi kuhusu viumbe hawa, tunazidi kuelewa uzuri wa sayari yetu tunayoishi.
Zipo tabia nyingi sana za Wanyama mbalimbali na tukisema tuchambue zote basi hatutoweza kumaliza hata kidogo
Writer - Kevin
Phone no - 0616152067






























Comments